Kitabu hiki ni mkusanyiko wa insha nilizoandika mwaka 2009 na kuzichapisha katika gazeti la KWANZA JAMII. Vile vile kuna mahojiano niliyofanyiwa na blogu ya Bongo Celebrity, mwaka 2008. Kwa ujumla, yaliyomo ni mawazo kuhusu masuala mbali mbali ya uchumi, siasa, jamii, na utamaduni yanayoihusu Tanzania na dunia kwa ujumla.
Kitabu hiki ni tafsiri ya kitabu kiitwacho “Africans and Americans: Embracing Cultural Differences” ambacho kimekuwa maarufu tangu kilipochapishwa mwaka 2005. Lengo la kitabu lilikuwa kuwawezesha waAfrika na waMarekani kuelewana na kuepuka kutoelewana na migogoro inayotokana na tofauti za tamaduni. Wasomaji waTanzania na waMarekani walinihimiza kukitafsiri. Hatimaye, mwaka 2023 Mwafrika Merinyo aliamua kukitafsiri. Nami naona amefanya kazi nzuri sana.
For over 30 years, Africonexion has been bridging the cultural gap between Africans and Americans, empowering them to thrive in diverse environments.